Kuchagua hadhira lengwa
Miradi ya kupinga unyanyapaa inafaa kulenga kuboresha ufahamu, mitazamo na tabia ya hadhira lengwa ambayo inaweza kuleta tofauti kubwa katika maisha ya watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia. Watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia wanapaswa kuwa msingi wa kazi yoyote ya kupinga unyanyapaa. Kuhusika inaweza kujumuisha mazungumzo yanayoendelea na kuhusika katika kikundi cha msingi na pia fursa za kuhusika katika shughuli mara moja tu. Wakati wa kutambua hadhira, ni muhimu kuwaza maswali ya ni nani na ni nini inafaa kubadilika.
Kuhusiana na ni nani, mipango ya kupinga unyanyapaa inaweza kulenga, kwa mfano, wataalamu wa afya na wa jamii, wanahabari, watengeneza sera, viongozi wa kidini, na pia inahitaji kufanya kazi pamoja na familia na watu walio karibu na watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao ili kuwasaidia kuelewa na kutoa msaada na kupunguza mawazo ya kubagua na tabia za kutenga ambazo zina maana sana. Watu ambao wana nguvu nyingi au mamlaka kuhusu maamuzi ya maisha na fursa zinazopatikana na watu wanaishi na ugonjwa wa dementia wanafaa kupewa kipau mbele kama hadhira.
Kuhusiana na nini, ni muhimu kuwaza tabia na mitazamo ambayo ni ya kuumiza zaidi au ni ya kukiuka haki kwa kuzuia fursa na uzima wa watu wanaoishi na dementia. Je, kuna habari potovu, mawazo ya ubaguzi au dhana zisizo kweli ambazo zinachangia matendo haya yasiyo haki? Mambo haya yakitambuliwa, ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja na hadhira lengwa ili kubuni mikakati ya mabadiliko ambayo yanafaa mahali, kutumia lugha inayoeleweka na yanatolewa kwa njia ambayo itafikia hadhira lengwa.
Mkakati wa kusaidiana kati ya watu walio na ugonjwa wa dementia na wanahadhira lengwa unaweza kuruhusu wanahadhira lengwa kuchukua wajibu wa kutekeleza mabadiliko.
Kutumia zana ya mazungumzo inaweza kuwa ya msaada ili kutoa suluhu kuhusu jinsi ya kuleta mabadiliko na kuruhusu njia tofauti na nyingi ambazo zitatengenezwa kufikia mahali na hadhira.
Mwisho, ni muhimu kutafakari kuwa njia ambayo inalenga aibu inaweza kutofanya kazi kwani watu wanaweza hisi kuwa wanaambiwa jinsi ya kutenda na mara nyingine jambo hili linaweza kutia nguvu tabia hasi. Kama ilivyoelezwa kote katika mwongozo huu, mikakati ya kubadilika inafaa kujumuisha mawasiliano ya kijamii na kuzungumzia habari za kibinafsi ili kuwasilisha habari. Mara nyingine, inawezekana kuwemo wanahadhira lengwa (kwa mfano wataalamu wa afya) walio na ugonjwa wa dementia na ambao wanaweza kushiriki mambo ambayo wamepitia kutoka kwa mtizamo wa mwathirika.
Zungumza na watu walio na ugonjwa wa dementia ili kutambua malengo- tafakari nani (kwa mfano wataalamu wa afya na wa jamii) na ni tabia au mitazamo gani inahitaji kubadilika
Kuwa na usawa kati ya kufikia vikundi mashuhuri na walio na mamlaka na pia wanaowasiliana kwa karibu na watu walio na ugonjwa wa dementia na pia wako na mamlaka
Tambua marafiki na washirika ambao wanaweza kusaidia kufanyia kazi hadhira lengwa. Kama kwa mfano, mtu amechagua kulenga wataalamu wa afya, inaweza kuwa muhimu kufanya kazi na washiriki ambao pia ni wataalamu wa afya ili kufikia hadhira hii lengwa vilivyo
Ujumbe unafaa kupeanwa na watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia
Kusaidiana na marafiki au 'wandani' wa hadhara lengwa kunaweza kusaidia kubuni mkakati wa kubadilika ambao unawafikia. Hii inahusisha kutumia lugha au njia wanazoelewa na wako huru nazo.
Tafakari habari ambazo sio za kutoa suluhu wazi au zinazotegemea kuaibisha mtu anayetenga wengine kwani mara nyingine hizi hazifanyi kazi wakati watu wanaambiwa ni nini wanafaa kuwaza. Kufanya kazi pamoja na washirika kunaweza kuongeza hali ya umiliki na kuwezesha mawazo ya kina ili kupata mabadiliko ya maana.
Wataalamu wa afya na wa jamii
Wanahabari
Wanaobuni sera
Viongozi wa kidini au wa jamii
Familia