Utangulizi wa mwongozo wa STRiDE
Idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia inatabiriwa kuongezeka zaidi ya mara tatu, kutoka kwa watu zaidi ya milioni 50 kwa sasa hadi watu milioni 152 ifikapo 2050. Kuongezeka kwa idadi ya watu wanaougua dementia inaweza kusemekana kusababishwa, kwa kiwango fulani, na ongezeko la umri wa kuishi katika nchi zenye mapato ya chini ya na kati.
Mwongozo huu unatokana na mradi wa STRiDE (Strengthening Responses to Dementia in Low and Middle-Income countries). Una mizizi kutokana na sauti na mambo wanayopitia watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watu wanaowatunza, na kuongezea kwa ushahidi uliopatikana kutoka kwa mradi wa STRiDE kuhusu jinsi ya kupunguza unyanyapaa na kutengwa.
Ni juhudi ya ushirikiano ambayo imeundwa na watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia, watunzaji, watetezi na watafiti wanaohusika katika mradi wa STRiDE. Hii ni pamoja na sauti za watu wa Brazil, India, Indonesia, Kenya, Jamaica, Mexico, South Africa, na UK.
Madhara ya unyanyapaa mara nyingi yanaelezwa kuwa mbaya au mbaya zaidi kuliko madhara kutokana na ugonjwa huu. Kwa mtu binafsi, unyanyapaa unaweza kudhoofisha malengo ya maisha, kupunguza kuhusika katika shughuli za maana za maisha na kusababisha ubora wa maisha kuwa mbaya zaidi. Kwa kiwango cha jamii, inaweza kuathiri sera na kupunguza fedha zinazotolewa kwa ajili ya matibabu na msaada.Hapa, tunatoa zana tendaji kutoka nchi saba zenye mapato ya chini na ya kati ili kusaidia wengine kufikiria kuhusu athari za unyanyapaa na jinsi ya kukabili unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao. Tunashiriki mambo wanayopitia ya unyanyapaa na kutengwa na madhara yanayotokana na mambo haya kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na familia zao-hivi kueleza makovu ya uchungu yanayotokana na kuepukwa au kutengwa.
Unyanyapaa unapata maana kuwa tatizo la maarifa (kutojua), matatizo ya mtazamo (maoni hasi bila ukweli) na matatizo ya tabia (ubaguzi)2.
Zipo njia kutokana na ushahidi za kupunguza unyanyapaa na kutengwa zinazoonyeshwa kupitia baadhi ya masomo ya kesi za utafiti zinazoonyesha jinsi watu wanaoishi na unyanyapaa na watunzaji wao walikabili unyanyapaa katika maisha yao wenyewe.
Ilhali kugeuzwa kuafikia utamaduni na kutafsiriwa kwa njia yoyote ya kukabili unyanyapaa ni muhimu, pia tunapendekeza kutumia maarifa yaliyoko na raslimali ili kujifunza kutoka kwa kazi za kupinga unyanyapaa zilizofuzu katika maeneo mengine na tamaduni zingine na kutoka kwa nyanja tofauti na aina za magonjwa na kulemaa ambayo pia yanaathirika na unyanyapaa.
Matukio ya unyanyapaa na kutengwa yanapatikana kwa kawaida. Mwakani 2019, majibu kutoka kwa utafiti mkubwa zaidi wa ulimwengu kuhusu unyanyapaa unaotokana na ugonjwa wa dementia, pamoja na majibu 835 kutoka kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia yaliashiria kuwa 84% walipitia unyanyapaa na kutengwa katika sehemu moja ya maisha yao.
Mabadiliko ya kijamii ya aina hii yanahitaji juhudi za pamoja kwa viwango vingi. Lengo letu ni kuunda mazingiria ambamo watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao wanaishi maisha bora zaidi, kwa njia yenye maana na salama. Watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia wanafaa kuongoza maono haya ya jinsi ulimwengu usio na unyanyapaa ungekaa. Hata hivyo, mabadiliko ya maana yanahitaji mbinu za juu chini na chini juu. Tunahitajika kufanya bidii ili kugeuza sera, mazoea na kanuni mbaya za jamii zisizo haki na ambazo zimekita mizizi katika jamii.
Hili linaweza kutokea tu kwa kuwawezesha na kuwasaidia watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia, familia na watunzaji wao ili kukabili unyanyapaa na kutengwa. Hivi basi, pia tunazungumzia mapendekezo ya vitendo ya jinsi ya kuwahusisha watu walio na ugonjwa wa dementia na familia zao na maswala mengine ya kuzingatia wakati wa kurekebisha na kutekeleza mpango wa kupinga unyanyapaa.
Hatuwezi, hata hivyo, kutegemea watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao ili kutekeleza mabadiliko haya. Hivyo basi zana hizi pia ni za kuelimisha na kusaidia umma kwa jumla, wataalamu wa afya na wa kijamii na wengine kuhusu jinsi tunaweza kugeuza tabia na kuwa watetezi wa kupunguza unyanyapaa na kutengwa.
Tunatambua kuwa mitazamo hasi inachangia kutojua na unyanyapaa unaozingira ugonjwa wa dementia. Hata hivyo, kupitia kwa mwongozo huu, tunatoa wito wa kutenda wa kwenda zaidi ya kuboresha maarifa na kuongeza ufahamu na kwa jinsi tunaweza kugeuza tabia zakuumiza, kutotendewa haki na sera zinazokuza kujumuishwa. Kipengele muhimu cha kuafikia mageuzi haya ya kijamii ni kuwawezesha watu walio na ugonjwa wa dementia kuongoza mipango hii na tuzungumzie mikakati ya kufanya hivi.
Lengo letu ni kutoa raslimali pana na yenye nguvu ambayo ina misingi ya ushahidi uliopo ili kuwawezesha watu walio na ugonjwa wa dementia ili kupigana na unyanyapaa.
Tunataka kushiriki mwongozo huu kwa upana iwezekanavyo na ili kufanya hivi tunahitaji msaada wako. Pamoja na kushiriki mwongozo huu na wengine, tumeweka viungo katika hati hii ambazo zinakuruhusu kushiriki nukuu na raslimali kupitia kwa mitandao ya kijamii pamoja na twitter, LinkedIn na Facebook. Tafadhali bonyeza ishara za mitandao ya kijamii katika hati ambazo zinakuwezesha kushiriki kwa urahisi habari hizi na kutusaidia kukuza harakati hizi za kijamii pamoja ili kupunguza unyanyapaa!
#UsisahauMimiNiBinadamu
Marejeleo:
1GBD 2019 Dementia Forecasting Collaborators. Estimation of the global prevalence of dementia in 2019 and forecasted prevalence in 2050: an analysis for the Global Burden of Disease Study 2019. Lancet Public Health. 2022;7(2):e105. doi:10.1016/S2468-2667(21)00249-8
2G Thornicroft, D Rose, A Kassam, N Sartorius Stigma: ignorance, prejudice or discrimination? Br J Psychiatry, 190 (2007), pp. 192-193
3Evans-Lacko, S, Bhatt, J., Comas‐Herrera, A., D’Amico, F., Farina, N., Gaber, S., Knapp, M., Salcher-Konrad, M., Stevens, M., and Wilson, E. (2019). Attitudes to dementia survey. World Alzheimer Report 2019, Attitudes to dementia. London: Alzheimer's Disease International. https://www.alzint.org/u/WorldAlzheimerReport2019.pdf