Mifano ya kushinda unyanyapaa katika nchi tofauti za STRiDE
Watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watu wanaowatunza wanapitia unyanyapaa na kutengwa katika nyanja tofauti za maisha. Tulielezea mambo haya wanayopitia na madhara yake katika sehemu iliyopita.
Lengo letu kuu ni kuunda mazingira ambamo watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao wanaweza kuishi maisha bora kwa njia ya maana na salama. Hii inamaanisha kumaliza unyanyapaa. Hata hivyo, unyanyapaa unaashiria utamaduni na imani katika jamii ambazo zinaweza kuwa za kina na zenye historia ndefu. Hivyo basi, hata kwa juhudi za pamoja, aina hii ya mabadiliko ya jamii huchukua muda.
Kwa sababu hii, ni muhimu kuwezesha watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia pamoja na wanaowatunza, na kuwasaidia kukabili unyanyapaa na kutengwa kwa njia salama na ya maana. Tunakiri kwamba kazi hii inaweza kuchukua aina na mkondo tofauti. Tunatoa mifano chache kutoka kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao kuhusu jinsi walivyoshinda unyanyapaa na kutengwa katika maisha yao binafsi.
Ni mchakato mgumu kwa mtu kukubali kuwa anaugua dementia. Kuna unyanyapaa. Ninachotaka ni kwamba watu wasikutendee tofauti. Usinizungumzie kana kwamba simo katika chumba. Watu watazungumza kana kwamba haupo, ila jamaa na marafiki wako wataelewa. Ninashinda ugumu kwa kukubali utambuzi wangu. Kukubali kuwa nina ugonjwa wa dementia. Jamaa wangu wa karibu na marafiki wanaelewa na hili linanisaidia kwa kiwango kikubwa. Msaada huo. Mwanzoni, sikukubali. Niling'ang'ana. Lakini nikaanza kushinda. Unachohitaji kufanya ni kukubali, na kutenda uwezavyo kila siku. Kukubali ni jambo kubwa katika kushinda unyanyapaa. Nikaanza kuambia watu kuwa hii ndio hali yangu. Hivi ndivyo ilivyo, na haitabadilika. Kuambia watu kwamba hii ndio hali niliyo nayo. Nikikosea, nisamehe. Iwapo ulisema utanitembelea au kukutana na mimi mahali fulani, nikumbushe. Mtu hafai kukasirika akikumbushwa. Nilikuwa nachukia kukumbushwa, lakini sasa sio hivyo. Keti na kupanga na kusema, kesho nitafanya hivi. Jiandikie maelezo. Huwa nacheza michezo, kwa mfano ya kutafuta maneno, nafanya vibaya sana katika michezo hii lakini nikiendela kucheza, nimegundua kwamba inanisaidia kukumbuka mambo. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwangu.
Bado nina mda wa kukaa na mke wangu. Hatuoni unyanyapaa kama jambo mbaya, tunaona tu kuwa ni changamoto na hatua ingine ya maisha.
Ufahamu pia unaweza kuenezwa katika mashule wakati wa mikutano ya wazazi shuleni. Hii ni njia mwafaka ya kufikia wazazi wengi kwa mara moja na kuwafunza. Habari pia inaweza kuenezwa makanisani, ili kuhakikisha kuwa imesambaa kote katika jamii.
Ndio, napaswa kuwasaidia [watu wanaotunza watu walio na ugonjwa wa dementia] kwa kuwapa ujasiri kutokana na mambo ambayo nimejifunza kutoka kwa mama. Nikifanya hivi, itakuwa changamoto kwao kufungua roho...
Ufahamu unaweza kuenezwa kupitia mazungumzo ya jamii.
...watu wanahitaji kupendwa, wanahitaji kutunzwa na hivi unafaa kuwasikiliza. Kadri unavyojua, unafaa kuwapa nafasi ya kuwa mtu ambaye wanataka kuwa, hivi basi unahitaji kuwa na subira nao, kuwaelewa na kuwasikiza
Mwanzoni, tulikuwa tunahepuka mikutano ya kijamii na kutompeleka mamangu nje, kama kwenda sokoni na kwingine, lakini tuligundua kwamba sisi wenyewe tulikuwa tunamuumiza na kuchangia unyanyapaa wake kwa kumficha na kutoeleza ugonjwa wake kuwa ana ugonjwa wa dementia. Ilituchukua muda kubadili mawazo yetu kuhusu hili jambo lote. Hivi sasa huwa tunampeleka kwa manyumba ya jamaa, mikutano ya hadhara na kueleza watu ugonjwa wa dementia ni nini. Kwamba ni ugonjwa wa akili na kuna dalili nyingi. Tunabagua kiasi swala la kumpeleka kwa manyumba ya watu kwani wengi bado hawaelewi tabia yake au wanakataa tu kuelewa ugonjwa wa Dementia au wako na mawazo yao binafsi kuhusu ugonjwa huu.