Kesi ya utafiti ya kupunguza unyanyapaa Kenya
Katika nchi zenye mapato ya chini na ya kati, nchi za Africa kusini mwa Sahara zina viwango vinavyoongezeka kwa sasi zaidi vya watu wanaozeeka (Alzheimer’s International, 2017). Nchini Kenya, idadi ya watu walio na umri wa miaka 60 na zaidi ilikuwa 4.3% mwaka wa 2017. Inatarajiwa kufika 10.6% mwakani 2050 (United Nations, 2017). Hivi sasa hakuna takwimu rasmi za idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia, ila inakadiriwa kuwa inawezekana watu 86,000 au zaidi wanaishi na ugonjwa wa dementia nchini Kenya, zaidi ya kuogezeka mara nne kufika 361,000 ifikapo 2050 (GBD 2019 Dementia Forecasting Collaborators, 2022).
Nchini Kenya, ugonjwa wa dementia unaonekana kama “ugonjwa wa Ulaya”. Hivyo, watu wengi wanaoishi na ugonjwa huu nchini Kenya hawatafuti utambuzi au msaada. Wakati watu wanatafuta utambuzi, wanakumbwa na mifumo ya afya iliyozidiwa pamoja na ufahamu wa chini au mawasiliano ya chini. Kutokana na haya, watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao wanaokumbana na mifumo hii wanawezakuhisi kupotea na kukosa matuamini.Katika jamii, dalili zinazohusiana na ugonjwa wa dementia mara nyingi zinadunishwa na kuonekana kama sehemu kawaida ya kuzeeka. Wakati dalili zinatambulikana, maneno yanayotumika ( kama Thing’ai/ kiburi 1) yanaweza kusambaza hadithi na dhana potovu kuhusu dementia.
Vigezo hivi vyote vinachangia unyanyapaa katika viwango vya kibinafsi, jamii na jumuiya Kenya. Mahojiano ya watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao yanaonyesha nyakati nyingi za unyanyapaa wa hadharani, kutengwa na mafikira ya kubagua.
1Jina linalohusiana na watu wanaoenda mjini kuchuma hela na kurudi vijijini wakishastaafu na kujitenga na jamii.
Ni wazi kuwa kuna athari kubwa ya unyanyapaa kwa maisha ya watu wanaoishi na dementia na watunzaji wao nchini Kenya. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa wale wanaoishi na unyanyapaa na kutengwa wako na suluhisho-wanahitaji tu kuulizwa. Mazungumzo yetu na watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na walezi wao Kenya iliibua kuwa wanatambua kuwa kuongeza ufahamu ni muhimu sana katika kukabili unyanyapaa, na hii ilifaa kufanyika kwa kuanzisha mazungumzo katika jamii.
Kutengeneza mwongozo pamoja na watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia, walinzi wao na wanajamii
Ili kuunda mwongozo wa mafunzo katika sehemu za vijijini Kenya, tulianza kwa kufanya kazi pamoja na jamii, sana sana watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na walinzi wao, kuelewa mitazamo, raslimali na malengo ya kupunguza unyanyapaa. Kwanza, ilibidi tuongee na kiongozi wa eneo kabla ya kuanza mradi. Baadaye tulikuwa na mazungumzo ya vikundi na mahojiano na watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia, watunzaji wao, wafanyi kazi wa afya na wanajamii kwa jumla.
Mazugumzo haya yalitusaidia kuelewa maarifa yaliyomo, mitazamo na tabia kuelekea watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao. Matukio ya unyanyapaa na kutengwa, lugha ya eneo kuhusu ugonjwa wa dementia, matendo ya sasa yanayochangia kujumuishwa kijamii na mawazo ya jinsi ya kupunguza unyanyapaa na kuwezesha watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao.
Tulibuni mafunzo na njia za kufunza kutokana na mazungumzo haya. Mafunzo yetu pia yalifaidika na mbinu zilizopo kutokana na ushahidi za kukabili unyanyapaa, (kwa mfano kugeuza mawazo kwa kujumuika kwa kikundi) na ujuzi uliomo ndani ya jamii ya kutoa mafunzo kwa jamii. Kwa mfano, tulitumia mbinu ya 'kufunza mkufunzi' pamoja na wahudumu wa eneo wa afya, ambayo ilituwezesha kuongeza kuhusika kwa wanajamii katika kutoa mafunzo.
Tulitengeneza video za 'kukutana kijamii' ambapo watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na walinzi wao kutoka jamii walieleza habari zao za kibinafsi kuhusu dementia, matukio ya unyanyapaa na jinsi waliyakabili. Pia tulitafuta maoni zaidi kuhusu mambo ya kina kama muundo, utoaji na idadi ili kusafisha mwongozo.
Muhtasari wa Vipengele vya mwongozo wa kupinga unyanyapaa Kenya
Katika utafiti wa mwanzo, tulipima mitazamo kuhusu dementia mbele ya na mwezi mmoja baada ya mafunzo kupeanwa kwa umma. Hii ilitiwa nguvu na hojaji za ubora.
Kati ya watu wa umma kwa jumla walioshiriki katika utafiti wa mwanzo, matokeo yaliashiria kuboreka kwa ufahamu na mitazamo kuelekea watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia pamoja na watu wanaowatunza.
Matokeo haya yaliungwa mkono na maoni ya ubora, kuonyesha kuwa mafunzo yalifanikiwa katika kuboresha ufahamu na kuondoa unyanyapaa.
Kilichokuwa cha kushangaza sana kwangu kuhusu dementia ni kuwa ni ugonjwa. Kwa muda mrefu, tuliamini kuwa sio ugonjwa. [Mwanzoni] tulifikiria watu wamerogwa au walikuwa wapumbavu tu.
Nilijifunza kutoka kwa mafunzo kuwa, naweza kubali huyu mtu anisaidie [Kwa kazi Fulani]. Kwa mfano, wakati wa kutayarisha chakula, anaweza nisaidia kuchagua mahindi, mbaazi
Tulikuwa na fikira kuwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia wanaadhibiwa kwa matendo yao mabaya ila sasa najua kuwa sio kupenda kwao.
Baada ya mafunzo, nilijifunza kuwa nahitaji kujua kutoka kwake ni nini angependa kula. Sasa hivi maisha si ngumu jinsi ilivyokuwa awali. Sasa hivi ni rahisi kumlinda na kumsaidia kuliko awali.
Alzheimer’s Disease International. (2017). Dementia in sub-Saharan Africa: Challenges and opportunities.
GBD 2019 Dementia Forecasting Collaborators. (2022). Estimation of the global prevalence of dementia in 2019 and forecasted prevalence in 2050: An analysis for the Global Burden of Disease Study 2019. The Lancet. Public Health, 7(2), e105.https://doi.org/10.1016/S2468-2667(21)00249-8
United Nations. (2017). World Population Ageing 2017—Highlights (ST/ESA/SER.A/397). Department of Economic and Social Affairs Population Division.