Kesi ya utafiti kuhusu kupunguza unyanyapaa nchini Brazil
Brazil ni nchi yenye mapato ya kiwango cha juu cha kati ambayo ina idadi ya watu takriban milioni 214 (Brazilian Institute of Geography and statistics, 2022; The world Bank, 2020) ambao 57% ni wanawake, na karibu 16% wako na umri wa miaka 60 na zaidi. (Brazilian Institute of Geography and Statistics, 2019). Nchi hii imegawanyika katika vikundi tano vya kijiografia (Kaskazini, Kusini, Kaskazini Mashariki, Kusini mashariki na Kati ya magharibi) na utofauti wa tamaduni na wasifu wa kijamii na kiuchumi. Kuzeeka kwa idadi ya watu kunafanyika kwa mojawapo ya viwango vya kasi sana kote ulimwenguni, ikipelekea ongezeko la watu wanaoishi na magonjwa sugu, pamoja na ugonjwa wa dementia (Melo et al, 2020, The World Bank ,2011). Makadirio kutoka mwaka wa 2019 yanaonyesha idadi ya watu milioni 1.8 wanaishi na ugonjwa wa dementia nchini humo (GBD,2022).
Unyanyapaa na kutengwa kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na wale wanaowatunza upo Brazil katika viwango tofauti, ikiwa ni pamoja na kati ya wataalamu wa afya (Oliveira et al., 2021) pamoja na wanajamii na familia za watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia (Oliveira et al., 2021).
Kwa sababu hiyo, watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia mara nyingi wanatengwa kijamii, na wale wanaowatunza mara nyingi huathirika. Kuongeza maarifa na ufahamu kuhusu dementia kati ya watu nchini Brazil ni muhimu. Kwa hivyo, huduma zinazolenga umma na jamaa za watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia zinaweza kusaidia kupunguza unyanyapaa na mawazo hasi kuhusu ugonjwa huu.
Lengo
Kuboresha ufahamu na mitazamo, na kupunguza unyanyapaa na kutengwa kutokana na ugonjwa wa dementia kwa wahudumu wa afya wa jamii.
Mbona wahudumu wa afya wa jamii?
Huduma za matibabu ya msingi ndio mwanzo wa kufikiwa kwa watu walio na matatizo ya afya ya mwili au ya akili nchini Brazil. Katika maeneo mengi nchini, vitengo vya huduma ya msingi ni sehemu ya mpango (Mkakati wa afya ya familia) na wahudumu wa afya wa jamii ni sehemu nyeti ya vikundi vya afya. Wataalamu hawa wanawajibika kwa kukuza afya na shughuli za kuzuia magonjwa, na kwa hivyo wahudumu wa afya wa jamii wanafanya kazi moja kwa moja kusaidia kuongeza kupatikana kwa huduma za msingi za afya kote nchini.
Mafunzo mengi ambayo yanatolewa kwa wahudumu wa afya wa jamii nchini Brazil yanalenga kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kama ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu bila kuzingatia sana mahitaji ya afya ya akili.
Mafunzo
Mafunzo yanajumuisha vipindi tatu vya vikundi, ambavyo vinawekwa siku tatu mfululizo, na kuchukua muda wa masaa matatu kwa kipindi, na ambayo yanahusisha wahudumu wote wa afya ya jamii ambao wanahusika kutoka kwa kila kitengo cha afya ya msingi katika kila kipindi (jumla=masaa 9 kwa siku 3 kwa wahudumu wote wa afya wa jamii).
Mafunzo yanatumia nakala za kuona na kusikia, na za kuchapishwa, ambazo kwa mfano zina video ya watu walio na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao wakishiriki mambo waliyopitia wao binafsi, mazoezi ya kutafakari, mazungumzo ya kikundi, na utoaji wa mafunzo kwa power point.
Lengo moja la mafunzo haya ni kushiriki jinsi ingekuwa kuishi na ugonjwa wa dementia
Siku ya 1 Kujenga ufahamu na kubadilisha imani: Kuanzia mchakato wa mabadiliko. Kipindi cha kwanza kinaanza na kipindi cha kumbukumbu za kunata. Wahudumu wa afya wa jamii wanaulizwa kutafakari kuhusu imani zao na mashaka yao, pamoja na ya washiriki wenzao na kujibu maswali yafuatayo:
Ugonjwa wa dementia unapatikana kutokana na…
Watu walio na ugonjwa wa dementia ni…
Kwa maoni yako, watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia wanafaa kutendewa vipi na watu wengine?
Kisha, tunapitia majibu kwa pamoja kama kikundi, kufanya mazoezi ya ziada ili kujenga urafiki, na baadaye kuuliza wahusika kuwaza:
"Je, umewahi fikiria jinsi maisha yako yangekuwa kama ungepata utambuzi wa kuwa na dementia?"
Siku ya 2 Kuvunja mawazo ya ubaguzi na kujenga mtazamo mpyaTunatoa mafunzo na habari ya kinadhari kuhusu unyanyapaa, kutengwa, mawazo ya ubaguzi na lugha ili kuwafunza wahudumu wa afya wa jamii jinsi mawazo ya watu wengine, hisia, mitazamo na tabia zinaweza kuathiri watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia. Kisha, tunaonyesha video za ushuhuda za watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia, na mwishowe tunakuwa na mazugumzo pana kusaidia wahusika kuwa na huruma kuhusu maswala ya kila siku ambayo yanapitiwa na watu walio na ugonjwa wa dementia.
Siku ya 3 Kuunganisha na mawasiliano ya kijamii na kuzungumzia njia za kuhusiana na wengine, kutenda, na hisia
Pia tunashiriki habari za maisha ya kila siku ya watu walio na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao, kutokana na hali za maisha halisi.
Tunafunza wahudumu wa afya mikakati bora ya mawasiliano ya maneno na yasiyo ya maneno, na kuanzisha tafakari na mijadala kuhusu jinsi ya kutumia mikakati hii katika maeneo yao ya kazi. Wahudumu wa afya wa jamii wanaulizwa kujaribu kujua usemi na tabia zisizofaa, na kuwaza uwezekano wa jinsi kila hali ingegeuzwa kuwa bora kwa kutumia mikakati bora ya mawasiliano ambayo ilifunzwa awali.
Kufunga na kutafakari jinsi habari za kupinga unyanyapaa zinaweza kujumuishwa katika kazi zao za kliniki.
Mjadala wa kikundi / tafakari kuhusu jinsi wahudumu wa afya wa jamii wanaweza kuboresha kazi yao ili kutoa matibabu bora zaidi kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na familia zao.
Kumbuka: Mwongozo na njia ya kupeana mafunzo inapatikana hapa. https://bmjopen.bmj.com/ content/12/7/e060033 sasa hivi tunatathmini mwongozo na tutaweka hapa raslimali hii pamoja na matokeo yakiwa tayari.
Brazilian Institute of Geography and Statistics. (2020). Nova proposta de classificação territorial mostra um Brasil menos urbano | Agência de Notícias. Agência de Notícias - IBGE. https://agenciadenoticias.ibge.gov.br/agencia-noticias/2012-agencia-de-noticias/noticias/15007-nova-proposta-de-classificacao-territorial-mostra-um-brasil-menos-urbano
Brazilian Institute of Geography and Statistics. (2022). IBGE | Projeção da população. https://www.ibge.gov.br/apps/populacao/projecao/box_popclock.php
Brazilian Institute of Geography and Statistics, B. (2019). Pesquisa Nacional de Saúde 2019: Ciclos de Vida. https://biblioteca.ibge.gov.br/visualizacao/livros/liv101846.pdf
Brazilian Ministry of Health. (2013). Pesquisa Nacional de Saúde 2013: Acesso e Uitlização dos Serviços de Saúde, Acidentes e Violências. https://biblioteca.ibge.gov.br/visualizacao/livros/liv94074.pdf
Brazilian Ministry of Health. (2019). Sistema Único de Saúde (SUS): Estrutura, principios e como funciona.http://www.saude.gov.br/sistema-unico-de-saude
GBD. (2022). Estimation of the global prevalence of dementia in 2019 and forecasted prevalence in 2050: An analysis for the Global Burden of Disease Study 2019. The Lancet Public Health, 0(0). https://doi.org/10.1016/S2468-2667(21)00249-8
Melo, S. C. de, Champs, A. P. S., Goulart, R. F., Malta, D. C., & Passos, V. M. de A. (2020). Dementias in Brazil: Increasing burden in the 2000–2016 period. Estimates from the Global Burden of Disease Study 2016. Arquivos de Neuro-Psiquiatria, 78, 762–771. https://doi.org/10.1590/0004-282X20200059
Oliveira, D., Mata, F. A. F. D., Mateus, E., Musyimi, C. W., Farina, N., Ferri, C. P., & Evans-Lacko, S. (2021). Experiences of stigma and discrimination among people living with dementia and family carers in Brazil: Qualitative study. Ageing & Society, 1–22. https://doi.org/10.1017/S0144686X21000660
The World Bank. (2011). Growing old in an older Brazil. http://documents1.worldbank.org/curated/ru/906761468226151861/pdf/644410PUB00Gro00ID0188020BOX361537B.pdf
The World Bank. (2020). Data for Brazil, Upper middle income country. https://data.worldbank.org/?locations=BR-XT