Kesi ya utafiti kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa dementia na mitazamo nchini Indonesia
Katika STRiDE, tulikuwa na utafiti mkuu nchini Indonesia. Tulichagua bila mpangilio watu 2110 ambao ni wazee katika Jakarta na Sumatra Kaskazini. Pia tulihoji mwanafamilia, rafiki au mtu ambaye alimfahamu mzee vizuri. Kutokana na haya, tuna data kutoka kwa watu karibu 4220 ambao wanaishi Indonesia, ambayo inahusiana na ufahamu wa dementia na mitazamo, ambayo ndiyo data kubwa zaidi ya aina hii. Hapa, tutaripoti kuhusu vigezo nne husika.
Idadi kubwa mno ya wahusika (n=3,780, 89.6%) walikubali au walikubali kabisa msemo kuwa "tunahitaji kuwa na uvumilivu zaidi kwa watu walio na ugonjwa wa dementia katika jamii yetu", na chini ya 5% kukanusha msemo huu (n=194).
Kadri ya nusu ya wahusika walihisi kuwa watu walio na ugonjwa wa dementia wanaweza kufurahia maisha (n=2,305, 54% walikubali au kukubali sana). La kuhusiana/muhimu zaidi, zaidi ya nusu ya wahusika (n=2,115; 50.1%) walihisi kuwa watu walio na ugonjwa wa dementia hawawezi kuchangia jamii vizuri.
Tokeo kuu la unyanyapaa ni kuwa watu wanaweza kuficha wengine utambuzi wao. Watu zaidi ya robo walisema wanaweza ficha utambuzi wao (n=1,069).
Matokeo haya ya mwanzo yanaashiria kuwa wengi wa watu wa Indonesia ndani ya sampuli yetu walikuwa na mitazamo kuhusu dementia ambayo inawezaonekana kuwa nzuri. Haswa kulikuwa na maoni ya nguvu kuwa tunafaa kuwa wavumilivu zaidi kwa watu wenye dementia katika jamii, ambalo ni jambo lenye ahadi.
Muhimu, kwa mambo fulani kulikuwa na idadi ya wachache wengi kiasi ambao walikuwa na maoni ya unyanyapaa zaidi ambayo yanaweza pelekea watu kuficha utambuzi wao au kuwa na tabia za matibabu ambazo haziboreshi maisha ya watu walio na dementia. Kulikuwa na jambo moja (" sifikirii watu walio na dementia wanaweza kuchangia vizuri katika jamii") ambayo ilionyesha kuwa mawazo fulani ya uongo na ya ubaguzi yanaweza kuwa yameenea.
Uchambuzi zaidi unahitajika ili kuweka muktadha kwa matokeo haya, ila kukusanywa kwa data kutoka kwa watu kuhusu mitazamo inatusaidia kufahamu mitazamo na imani ambazo zinaweza kuwa za unyanyapaa, pamoja na kupeana fursa ya kuelewa ni nani na ni kwa nini vikundi fulani vinaweza kuwa na mitazamo hii.