Mawasiliano ya kijamii na mawasiliano pepe ya kijamii
... video kutoka kwa kila nchi
Mawasiliano ya kijamii ni mawasiliano ya moja kwa moja na ya kibinafsi kati ya umma kwa jumla na watu kutoka kwa kikundi kilichopitia unyanyapaa, kama watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao. Njia hii ni mojawapo ya njia zinazofanya kazi vyema zaidi katika kupunguza unyanyapaa na kutengwa na utafiti mwingi umetoa ushahidi wa njia hii.1,2
Mawasiliano ya kijamii yanaweza fanya kazi kwa mviringo mwema, pale watu wakizungumzia kwa wazi kuhusu dementia inapunguza hadithi na imani potovu, kupelekea kupungua kwa unyanyapaa katika jamii, na hivyo kuwa na mazingira ya msaada zaidi kwa watu kueleza kuhusu kuwa na dementia na kuvunja zaidi unyanyapaa na kutengwa. Kwa kweli mawasiliano ya kijamii yanakuwa ya kukumbukwa zaidi na kudumu zaidi kuliko mafunzo ya kielimu.
Utafiti unaonyesha kuwa baada ya muda, watu husahau ukweli na takwimu ila athari za hadithi za kibinafsi zinaleta mabadiliko ya muda mrefu kwa watu.
Ili kufanikiwa, mawasiliano ya kijamii yanafaa kuwa zaidi ya kuleta watu pamoja. Yanafaa kutoa fursa za maana kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na watunzaji wao kushiriki mambo wanayopitia, kuanzisha mijadala na kubadilisha mawazo. Ubora wa mawasiliano ya kijamii ni bora kuliko idadi/kiwango. Kuna mambo matano yanayosaidia kuwa na mawasiliano ya kijamii ya maana na ambayo yanaweza kuongeza ukaribu na uwezekano wa urafiki pamoja na kupunguza uoga 3. Haya ni pamoja na:
Hali sawa kati ya vikundi (vya watu walio na wasiokuwa na dementia)
Kufanya kazi kuelekea lengo la pamoja
Kushirikiana kati ya vikundi
Msaada wa mamlaka, sheria au desturi.
Uwezekano wa urafiki
Shughuli au matukio ya mawasiliano ya kijamii yanafaa kulenga kueneza mambo hayo tano.
Kwa sababu hali ya mtu ya dementia sio jambo ambalo linaweza kuonekana wazi, kusema au kushiriki hali ya mtu ni jambo la maana sana katika tukio la mawasiliano ya kijamii. Kwa sababu hii, ni muhimu kuwa na mazingara bora ambayo yanasaidia mtu kusema hali yake ya dementia na kusaidia watu kwa mchakato wote wa ni nini na ni kwa jinsi gani wanafaa kushiriki na pia kuhakikisha wanapata msaada katika na baada ya tukio na kuhakikisha kuwa wanafanyiwa heshima.
Kuwasiliana kwa kijamii kunaweza kufanyika kupitia matukio ya moja kwa moja ya mikutano au mikutano ya kimtandao, au video au filamu. Ilhali mawasiliano ya kijamii ya moja kwa moja ndio njia ya fanaka zaidi, mara nyingine haiwezekani. Kuna ushahidi kuwa mawasiliano ya kijamii pia yanaweza kupatianwa kupitia kwa mtandao, filamu au video ya mahojiano. Pia yanaweza kujumuisha shughuli za kujifurahisha ambazo zinahitaji kazi ya pamoja na ushirikiano wa watu wanaoishi na ugonjwa wa dementia na umma kwa jumla au vikundi vingine vilivyolengwa.
Pia kunayo mifano mingine ya kisanaa ya kuwa na matukio ya moja kwa moja kama Human Libraries ambapo watu walio na utambulisho wa unyanyapaa wanaweza “twaliwa” na kutumia mazungumzo na mambo ya kibinafsi yaliyopitiwa ili kukanusha hadithi na mawazo hasi na pia kujenga urafiki. (https://humanlibrary.org/). Ni muhimu kuwa shughuli iliyochaguliwa inasaidia mjadala, kushiriki mambo yaliyopitiwa na mazungumzo.
Marejeleo:
1 Al Ramiah A, Hewstone M. Intergroup contact as a tool for reducing, resolving, and preventing intergroup conflict: evidence, limitations, and potential. Am Psychol. 2013 Oct;68(7):527-42. doi: 10.1037/a0032603. PMID: 24128316.
2 National Academies of Sciences, Engineering, and Medicine. (2016). Ending Discrimination Against People with Mental and Substance Use Disorders: The Evidence for Stigma Change. Washington, DC: The National Academies Press. doi: 10.17226/23442
3 Brown, R., & Hewstone, M. (2005). An integrative theory of intergroup contact. Advances in Experimental Social Psychology, 37,255–343. doi:10.1016/S0065-2601(05)37005-5
4 Janoušková, M., Tušková, E., Weissová, A., Trančík, P., Pasz, J., Evans-Lacko, S., & Winkler, P. (2017). Can video interventions be used to effectively destigmatize mental illness among young people? A systematic review. European Psychiatry, 41(1), 1-9. doi:10.1016/j.eurpsy.2016.09.008
Brazil
Indonesia
India
Kenya
Jamaica
Jamaica
South Africa
Bonyeza chati ili kuona nakala kamilifu